Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha shilingi
milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule ya sekondari ya Wasichana ya
Ruvu iliyopo Kibaha vijijini mkoani Pwani.
Akizungumza wakati
alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia katika Harambee hiyo ambayo ilifanikiwa
kukusanya kiasi cha shilingi milioni 510 kati ya shilingi milioni 700
zinazohitajika , Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia anaunga mkono
uamuzi huo wenye nia ya kuwafanya wanafunzi katika shule hiyo kusoma katika
mazingira salama.
Katika hatua nyingine
Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa halmashauri nchini kuendelea kutenga fedha
kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa shule katika
maeneo hayo badala ya kusubiri Serikali kuu pekee.
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa Ujenzi ambaye pia ni Katibu wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amos Makala amesema lengo la kukusanya fedha hizo
ni kuhakikisha wanajenga uzio huo ili kuwapa usalama watoto wa kike wanaosoma
katika shule hiyo.
Harambee hiyo
imefanyika jana Jumamosi (Juni 14, 2025) jijini Dar es Salaam.
0 Maoni