Wakala wa Huduma za Misitu
(TFS) imeanzisha kampuni tanzu ya “Misitu Company Ltd”, ambayo pamoja na mambo
mengine itajikita katika uendeshaji wa baadhi ya viwanda na biashara ya mazao
ya nyuki.
Kampuni hiyo
itakapokamilisha taratibu za uendeshaji itakuwa tayari kununua mazao ya nyuki
kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wananchi watakaohudumiwa na Kiwanda cha
Asali cha Sao Hill.
Haya yamebainishwa na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa
akijibu swali la Mhe. Ritta Enespher Kabati ambaye alitaka kujua Kiwanda cha
Asali cha Sao Hill kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kitanunua
Asali kutoka kwa Wananchi?
Mhe. Kitandula
alisema Kiwanda cha kuchakata asali cha Sao Hill kwa kuanzia kinatoa huduma za
uchakataji wa mazao ya nyuki yanayozalishwa na TFS pamoja na wananchi kutoka
vijiji jirani.
“Hata hivyo, kwa sasa
kiwanda hakijaanza kununua mazao ya nyuki ikiwemo asali kutoka kwa wananchi kwa
kuwa mfumo wa uendeshaji wa Wakala za Serikali hautoi mwanya huo kibishara,” ameeleza
Mhe. Kitandula.
Na. Anangisye
Mwateba - Dodoma
0 Maoni