Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini
(TARURA) Mhandisi Victor Seff amewaagiza Mameneja wa Mikoa nchi nzima kuanza
kutangaza zabuni za mwaka wa fedha 2025/26.
Mhandisi Seff ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi ya
Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida pamoja na kuzungumza na Mameneja wa TARURA wa
wilaya katika mkoa huo.
Amesema katika zabuni hizo zizingatie barabara zenye
kipaumbele kwa wananchi na zile zenye changamoto za kupitika
Pia Mtendaji Mkuu huyo aliwasisitiza Mameneja kufanya
matengenezo ya barabara kwa wakati
na kuhakikisha miradi yote ya kwenye
maeneo yao inaanza mapema.
Hata hivyo amewataka Mameneja wa wilaya kuandaa mipango ya
kuboresha barabara kwa kuzingatia
vipaumbele.
Mhandisi Seff yupo Mkoani Singida ambapo jana tarehe 1 Mei, 2025 alishiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani na kupewa zawadi ya fedha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Mfanyakazi hodari wa TARURA kwa mwaka 2024/25.
0 Maoni