Ujumbe wa Tanzania kutoka Wizara ya Madini, ukiongozwa na
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, umewasili jijini London
nchini Uingereza jana kwa ajili ya kushiriki Jukwaa la Uwekezaji kwa Sekta ya
Madini lililobeba agenda ya Uongezaji Thamani Madini (Minerals Beneficiation
And Value Addition).
Jukwaa hilo ni fursa kubwa ya kuvutia wawekezaji wa kujenga
viwanda nchini Tanzania na kuondokana na
utegemezi wa kusafirisha madini ghafi jambo ambalo litasisimua ukuaji wa uchumi
na kuongeza ajira kwa Watanzania.
Ujumbe huo umepokelewa vizuri na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Mbelwa Kairuki, ambapo mazungumzo mafupi kuhusiana na vikao vinavyotarajia kuanza tarehe 20.05.2025 hadi 22.05.2025 yamefanyika.



0 Maoni