Prof. Silayo asaini mkataba wa kupokea msaada kutoka UNDP

 

Kushoto chini ni Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, akisaini Mkataba wa Makubaliano ya kupokea msaada kutoka kwa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), pamoja na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania, Shigeki Komatsubara. Msaada huo, wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 338, unajumuisha magari mawili aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop (5-seater) na pikipiki 20. Umetolewa kupitia mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuai ya Misitu dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi, uliotiwa saini kati ya UNDP na Wizara ya Fedha na Mipango kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 23 Agosti 2023. 

Hafla ya leo Mei 5, 2025 imefanyika katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia wa Pugu–Kazimzumbwi, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, na kushuhudiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb), pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi.





Chapisha Maoni

0 Maoni