Papa mpya Robert Prevost, ambaye atajulikana kama Papa Leo XIV, amekuwa Mmarekani wa kwanza kuchaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani.
Prevost, 69, ambaye baba yake anaasili ya Ufaransa na mama
yake Italia, amejitokeza baada ya kuchaguliwa na kuwasalimia maelfu ya watu
waliokusanyika St Peter's Square.
“Amani iwe kwenu wote,” alisema Papa Leo XIV akiwasalimu
watu akiwa kwenye kibaraza cha Vatican.
Prevost mzaliwa wa Chicago Marekani ni mwanamabadiliko na
amefanya kazi kwa miaka mingi kama mmishenari huko Peru kabla ya kuwa Askofu akiwa
huko.
0 Maoni