WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Mei 8, 2025 amehani msiba
wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Cleopa David
Msuya, Upanga Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine,
Mheshimiwa Majaliwa, amewasihi kuendelea kumuombea Mhe. Msuya na wawe
wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Marehemu Cleopa Msuya alifariki Mei 07, 2025 katika hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
0 Maoni