Majaliwa akutana na viongozi wa Wizara ya Ardhi ya Japan na wa JAIDA

 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa jana Mei 27, 2025, alikutana na Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan,  Mheshimiwa Hiromasa Nakano  kwenye Makao Mkuu ya Wizara hiyo Tokyo Japan.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta ya Miundombinu la Japan (JAIDA)  Miyamoto Yoichi pamoja na ujumbe wake ambapo walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji kwenye sekta za Ardhi, Miundombinu pamoja na Usafirishaji.





Chapisha Maoni

0 Maoni