Waziri Mkuu, Kasim
Majaliwa Mei 29, 2025 alikutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama
cha Wabunge wa Japan cha Urafiki na Afrika (Africa Union Parliamentarians
Friendship) Mheshimiwa Ichiro Aisawa, kwenye Ofisi za Bunge la Japan.
Katika mazungumzo yao
walijadili kuhusu kuendeleza urafiki kati ya Bunge la Tanzania na Bunge la
Japan.
Pia, walijadili
kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Japan,
pamoja na kumkaribisha kutembelea Tanzania ili kujionea vivutio
mbalimbali ya utalii.
0 Maoni