Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan
Abbasi amefanya ziara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kukagua utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwepo mradi wa Ujenzi wa Jengo la kisasa la
Makumbusho ya Jiolojia, Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya NCAA linalojengwa nje
ya Hifadhi ya Ngorongoro katika Wilaya ya Karatu.
Ujenzi wa Miradi hiyo imefikia zaidi ya asilimia 90 na
inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Dkt. Abbasi amesisitiza Menejimenti ya NCAA ikiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Dkt. Elirehema Doriye kuendelea kusimamia utekelezaji wa Miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati, kuzingatia thamani ya fedha na viwango vya kimataifa kwa ajili ya kuhudumia wageni.
0 Maoni