Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa - TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba
amepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi Mil.42.4 kwa ajili ya huduma
za Afya na Elimu kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha
kwa Jamii.
Akipokea vifaa hivyo Mhe. Katimba amesema serikali
inaendelea kuhakikisha inapeleka maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo
sekta ya Afya,Elimu na miundombinu hiivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea
kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.
“Tuwashukuru sana wadau wetu wakubwa wa NMB tunatambua
jitihada zenu za kuunga mkono serikali kwa juhudi kubwa zinazofanywa na
serikali ya awamu ya sita katika sekta nyingi ikiwemo Afya na Elimu,” amesema
Mhe. Katimba.
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Kaimu meneja wa NMB kanda ya
Magharibi Gardiel Sawe ni vifaa vya kujifungulia, Viti vitano (05) kwa ajili ya Wagonjwa, Vitanda
kumi (10) kwa ajili ya Wajawazito kujifungulia
ambavyo vyote vimetolewa kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Vitanda hamsini
(50) kwa Wanafunzi wa Shule za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Hata hivyo, vifaa vya Afya vitasambazwa na kunufaisha Kituo cha Afya cha Ujiji, Kituo cha afya cha Buhanda, Kituo cha afya cha Kikunku na Zahanati ya Bangwe.
0 Maoni