Waziri Mkuu kufanya ziara ya siku moja Nansio - Ukerewe mkoani Mwanza

 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo Aprili 25, 2025 amewasili mkoani Mwanza ambapo ataelekea Nansio-Ukerewe kwa ziara ya siku moja.

Akiwa katika kisiwa hicho Mhe. Majaliwa atakagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali yenye hadi ya Huduma za Rufaa ya Mkoa, ataweka jiwe la msingi la jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe pamoja na kufanya mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa Getrude Mongela.






Chapisha Maoni

0 Maoni