Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa za Maendeleo ndani ya Miaka 61 ya Muungano Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii na kuwa kielelezo cha Mafanikio ya Muungano Barani Afrika.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi la
Ujenzi Wa Barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es
Salaam ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa
Tanzania.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema Wananchi wa pande zote mbili
wanaendelea kunufaika na matunda ya Muungano tangu Kuasisiwa kwake na kufanikisha dhamira ya Waasisi wake Ya
Kuleta Uhuru,Umoja na Maendeleo ya Watanzania .
Rais Dkt. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan kwa Kuendelea Kuimarisha Muungano kwa
kuzipatia Ufumbuzi Changamoto za Muungano kwa kupitia vikao vya Pamoja vya
Majadiliano kama ilivyofanywa na Viongozi waliopita.
Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amefafanua kuwa Amani ya
kudumu na Umoja wa Watanzania ni Tunu Muhimu zinazopaswa kulindwa na kila
Mtanzania.
Akizungumzia Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara hiyo
aliyoiwekea Jiwe la Msingi na Miradi mingine ya Maendeleo ni matokeo ya kuwepo
kwa Amani na kuiwezesha Serikali kutekeleza Mipango ya Maendeleo.
Ametoa Wito kwa Watanzania Kuendelea kulinda Amani Ili Taifa
lipige hatua zaidi za Maendeleo na kwa
kuwa huu ni Mwaka wa Uchaguzi amewataka kutumia haki yao kuchagua Viongozi na
kuhakikisha Uchaguzi hauwi chanzo cha kuhatarisha Amani ya Nchi na kuweka Mbele
Maslahi ya Taifa.
Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi , Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia Jerry John Silaa amesema Barabara Hiyo itaifungua Wilaya ya Kigamboni
Kiuchumi na kuwaunganisha
Wananchi katika harakati za Kijamii.
Barabara Hiyo itagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 83.8 hadi kukamilika kwake inajengwa na Kampuni ya Estim Construction Limited.
0 Maoni