Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba
amewaelekeza wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za mitaa kutengeneza mchanganuo
na kubaini watumishi wangapi wanadai malimbikizo ya mishahara na yasiyo
yamishahara na kuyawasilisha Utumishi kuhakikiwa na kupekwa hazina kwaajili ya
malipo.
Ameyatoa maelekezo hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali
la Mhe. Bonnah Kamoli mbunge wa Segerea kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa, aliyetaka kujua serikali inampango
gani wa kulipa malimbikizo ya mishahara na marupurupu ya walimu.
Akijibu hilo Mhe. Katimba amesema “Naomba nitoe msisitizo
huo na jana kwenye bajeti ya wizara ya utumishi maelekezo hayo yalitolewa na
wizara hiyo na mpaka itakapo fika tarehe 31 Mei wakurugenzi wote wawe
wamewasilisha majina hayo ya watumishi hao ambao wanadai malipo yao” Amesema
Aidha, akijibu kuhusu mazingira bora ya walimu Mhe. Katimba amesema serikali inaendelea kujenga nyumba za walimu ili walimu wapate mazingira mazuri ya kuishi na kufanyakazi kwa ufanisi.
Na. OR - TAMISEMI
0 Maoni