Rais Mstaafu wa
Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha ujumbe maalum kwa Rais wa
Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Kikwete
amewasilisha ujumbe huo maalum, pembenzoni mwa Mkutano wa Uongozi wa Afrika wa
nane unaofanyika jijini Kampala nchini Uganda.
Kwa upande
wake Rais Museveni alimshukuru kwa ziara na kumuomba amfikishie salamu zake kwa
Mheshimiwa Rais Samia na watu wa Tanzania.
0 Maoni