Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
yuko mjini Boston nchini Marekani, ambako anashiriki katika kutoa mafunzo kwa
Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea.
Mafunzo hayo yanafanyika chini ya Mpango wa Uongozi wa Ngazi
ya Mawaziri wa Harvard, maarufu kama Harvard Ministerial Leadership Program,
unaoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ni mmoja wa Viongozi
Wakuu wa Kitaifa Wastaafu walioalikwa kushiriki kama wakufunzi, wakitumia
uzoefu wao wa uongozi kuhamasisha na kuwajengea uwezo viongozi wa kizazi kipya.
Mbali na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, mafunzo haya pia yanashirikisha Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, wawakilishi wa mashirika binafsi, pamoja na mabingwa wa masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka maeneo mbalimbali duniani.
0 Maoni