Aliyekuwa mwaandaji wa mashindano ya Miss Tanzania Hashim
Lundenga amefariki dunia asubuhi ya leo 19/04/1015 katika hospitali ya Kitengule
iliyupo Tegeta Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa Marehemu Lundenga, Bosco
Majaliwa, Lundenga ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu, alikimbizwa
hospitalini hapo leo asubuhi baada ya kuzidiwa lakini muda mfupi baadaye
akafariki.
“Hapa ndiyo tunafanya utaratibu wa kuuchukua mwili kwenda kuuhifadhi halafu turudi nyumbani Boko kupanga taratibu za mazishi,” alisema Bosco kwa masikitiko.
0 Maoni