Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mlezi wa Chama cha Mawakili wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi mpya wa Chama cha Mawakili wa Serikali (TPBA) kwa lengo la kuwapongeza viongozi waliochaguliwa, pamoja na kushuhudia zoezi la makabidhiano ya nyaraka muhimu za chama hicho.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
amekutana na viongozi hao, Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Jumatano tarehe
16 Aprili 2025.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali amewaahidi ushirikiano wa kutosha viongozi wapya wa Chama cha Mawakili
wa Serikali huku akiwa na akielezea
matumaini yake makubwa aliyonayo
kwa viongozi hao katika kuendeleza yale yaliyoachwa na uongozi uliomaliza
muda wao na kukipeleka chama hicho mbele zaidi.
“Mimi kama mlezi wa chama
hiki nawaahidi kuwapa ushiirkiano mkubwa na mtakapokuwa tayari na kujua nini
mnataka kufanya katika ile STRATEGIC PLANNING mnakaribishwa wakati wowote kwa
mlezi wenu ili niweze kuwapa hiyo support,” amesema Mwanasheria Mkuu wa
Serikali .
Aidha, Mhe. Johari
ameshuhudia makabidhiano kati ya Uongozi uliomaliza muda wake na uongozi mpya
wa Chama cha Mawakili wa Serikali.
Kwa upande wake, Rais wa
Chama hicho aliyemaliza muda wake Bw. Amedeus Shayo amesema kuwa ana Imani
kuwa, chama hicho kitaendelea kuwa imara kwakuwa kimepata viongozi makini wenye
maono mapana huku akiwaahidi kuwapa ushirikiano katika kuendelea kukijenga
chama hicho.
“Nawaahidi kuwapa
ushirikiano tuendelee kufanya kazi pamoja kwasababu kukijenga chama ni jukumu
letu sote,” amesema Bw. Shayo.
Naye Rais mpya wa Chama cha
Mawakili wa Serikali Bw. Bavoo Junus amemshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali
na Mlezi wa Chama hicho Mhe. Hamza S. Johari kwa maono yake ya kukiona chama
hicho kuwa kinakuwa Chama kikubwa katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Vilevile Bw. Bavoo amesema
uongozi wake umejipanga kutekeleza yale yote yaliyoanishwa kwenye mkakati wa
Chama hicho kwa viwango na weledi na ili kukifanya chama kufikia malengo
waliyojiwekea. Pia Rais huyo mpya amemshukuru Rais aliyemaliza muda wake kwa
kujenga misingi imara ndani ya chama hicho.
0 Maoni