CCM yapangua ratiba ya uchukuaji fomu wagombea

 

Chama cha Mapinduzi (CCM) chabadilisha tarehe ya kuanza mchakato wa ndani wa uteuzi wa wagombea nafasi za ubunge, ujumbe wa baraza la wawakilishi na udiwani kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Katika marekebisho hayo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi sasa mchakato huo wa uchukuaji fomu utaanza rasmi tarehe 28 Juni 2025, saa 2:00 asubuhi na kukamilika tarehe 2 Julai 2025, saa 10:00 jioni.



Chapisha Maoni

0 Maoni