DRC yasema hapana mazungumzo na M23 yaitaka Rwanda

 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekataa kufanya mazungumzo ya maridhiano na waasi wa kundi la M23, ambalo limeteka maeneo makubwa mashariki mwa nchi hiyo katika miezi ya hivi karibuni.

Uamuzi huyo wa DRC kugoma kufanya mazungumzo na waasi hao umetolewa licha ya shinikizo linalozidi kuongezeka kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kuitaka kufanya hivyo.

Wiki iliyopita, serikali ya Uingereza ilitoa wito wa kuhusisha kundi la M23 katika mazungumzo ya kujumuisha, kama sehemu ya juhudi za kupata suluhu ya kisiasa kwa mzozo huo.

Hata hivyo, katika mahojiano na BBC, Waziri Mkuu wa DRC, Judith Suminwa Tuluka, amesisitiza kuwa serikali yake inapendelea kuzungumza na Rwanda, nchi jirani ambayo inashutumiwa kwa kuuunga mkono M23.

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka za DRC, zaidi ya watu 8,500 wamepoteza maisha tangu mapigano yalipoongezeka mwanzoni mwa mwaka huu.

Chapisha Maoni

0 Maoni