Jeshi la
Polisi limemkamata Elia Asule Mbugi (25) marufu kama Dogo bata mkazi wa Segerea
dereva aliyekuwa akiendesha gari namba T 580 EAE aina TATA Daladala lililosababisha
kifo cha SP Awadh Ramadhani Chico aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya kipolisi
Chanika.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema mtuhumiwa huyo
alikamatwa na makachero wa Polisi Kanda
maalum ya Dar es Salaam tarehe 27 Machi 2025 maeneo ya Mbalizi Mkoani Mbeya, na
atafikishwa mahakamani haraka
iwezekanavyo.
Dereva huyo
alikuwa akisakwa na Polisi Jijini Dar es Salaam tangu tarehe 17 Machi 2025 ilipotokea ajali hiyo iliyosababisha
kifo cha SP Chico, kufuatia kutoroka
mara tu baada ya kugonga gari na kusababisha kifo.
0 Maoni