Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba ongezeko la ushuru kwa Mexico na Canada, litaletea maumivu, lakini yatakuwa na manufaa.
Nchi za Canada na Mexico nazo zitajibu mapigo kwa kuiongezea ushuru, baada ya Marekani, iliyoongeza kodi ya asilimi 25 kwa bidhaa za nchi hizo pamoja na kodi ya asilimia 10 kwa China.
China nayo imesema itatekeleza hatua za kujibu mapigo na
inampango wa kufungua shauri kwenye Shirika la Biashara Duniani.
Ongezeko la ushuru wa bidhaa litaanza kutekelezwa Jumanne,
ambapo Rais Trump amesema ni katika kukabiliana wahamiaji haramu na
wasafirishaji dawa za kelevya.
Jumuiya ya kimataifa imeonyesha kuguswa na kutoa maoni yao, ambapo Waziri wa Viwanda wa Ufaransa Marc Ferraci amesema, “nidhahiri tunapaswa kuchukua hatua”.
0 Maoni