Vatican imesema Papa Francis amepumzika vyema na usiku wa jana ulikuwa wa amani, baada ya taarifa ya Jumamosi kwamba alikuwa mahututi, akisumbuliwa na tatizo la kupumua mithili ya pumu.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani ilielezwa kuwa hali yake kuwa mbaya siku ya Ijumaa na aliongezewa damu.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 amekuwa akitibiwa nimonia kwenye mapafu yake yote mawili katika hospitali ya Gemelli huko Roma.
Imeelezwa kuwa Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani anajitambua na yupo kwenye kiti chake cha magurudumu, ila bado anategemea zaidi mfumo wa oksijeni akiwa chini ya uangalizi wa madaktari.
0 Maoni