Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
tarehe 8 machi, 2025 Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana
na kampuni ya Tanzania Coorporates imeandaa safari ya siku moja kwa wanawake
kutembeela vivutio vya utalii vilivyopo katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro.
Akitangaza kampeni hiyo jijini Arusha Kamishna msaidizi
Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya huduma za Utalii na Masoko
ameeleza kuwa Safari hiyo ya siku moja (Day Trip) itafanyika tarehe 7 Machi,
2025 kuanzia Jijini Arusha ambapo ina lengo la kuunganisha wanawake katika
sekta ya utalii ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kutangaza Utalii
wa ndani kwa kutembelea Kreta ya Ngorongoro.
“Kama mnavyojua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara namba moja kutangaza Utalii wa
vivutio tulivyokuwa navyo hapa nchini, mtakumbuka Filamu ya Tanzania the Royal
Tour na Amaizing Tanzania yeye ndio amekuwa Jasiri muongoza njia kutangaza
utalii wa nchi yetu duniani, kwa kuelekea siku hii tumeamua kuungana na
kuhamasisha wanawake kufanya utalii wa ndani katika eneo la hifadhi ya
Ngorongoro.
Mkurugenzi wa Tanzania Coorporates Elina Mwangomo ameeleza
kuwa gharama ya safari hiyo itakuwa shilingi 170,000 pekee kwa kila mtu ambapo
gharama hiyo itajumuisha kiingilio, chai ya asubuhi, chakula cha mchana,
usafiri, gharama za muongoza watalii pamoja na kila mshiriki kupewa kofia
atakayovaa wakati wa safari ya Utalii.
“Sisi kama wanawake wa Sekta ya Utalii tumeamua kumuunga
mkono Kama mnavyojua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara namba moja kutangaza Utalii wa vivutio
tulivyokuwa navyo hapa nchini, mtakumbuka Filamu ya Tanzania the Royal Tour na
Amaizing Tanzania yeye ndio amekuwa Jasiri muongoza njia kutangaza utalii wa
nchi yetu duniani.
kwa kuhamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kuungana
katika safari hii ya kufanya Utalii Ngorongoro ambapo tunaamini wote
watakaolipia kifurushi cha 170,000 kwenda kutalii Ngorongoro watapata uzoefu
mzuri usiosahaulika katika Maisha yao (unforgettable experience) na watarajie
kuona mtawanyiko wa wanyama mbalimbali ikiwemo Wanyama wakubwa watano ambao ni
Simba, chui, Faru, tembo na Nyati wakiwa katika mazingira ya asili na katika safari
hii watapata huduma ya usafiri uliopo katika kiwango kizuri na usalama wa
kutosha wakati wote wa safari.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Thabea Mollel amewahakikishia wanawake wote watakaoshiriki safari ya
utalii Ngorongoro watapata usalama wa hali juu katika safari ya utalii katika
hifadhi ya Ngorongoro na kurudi Arusha.
Wanawake ambao watahamasika kuunga mkono jitihada za utalii wa ndani wanaweza kupiga namba 0758171914 au Namba 0763 291179 kisha watapewa utaratibu.
Na. Kassim Nyaki - Arusha
0 Maoni