Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu amezindua huduma mpya
ya uwekezaji wa hisa kupitia Popote Mobile App.
Huduma hii itawawezesha wateja kununua, kuuza na kuangalia
mwenendo wa bei za hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Huduma hiyo mpya ambayo ni zao la ushirikiano kati ya benki
ya TCB na DSE, ilizinduliwa jana Ijumaa, Februari 21, 2025, jijini Dar es
Salaam.
Uzinduzi wa huduma hii unakuja katika wakati ambapo soko la
mitaji la Tanzania linahitaji mageuzi ya kidijitali ili kuongeza ushiriki wa
wananchi.
Popote Mobile App ni suluhisho la kisasa ambalo linaruhusu
Watanzania kufanya miamala ya hisa kupitia simu zao za mkononi, hali
itakayochochea ukuaji wa uchumi na kupanua fursa za uwekezaji katika masoko ya
mitaji.
0 Maoni