Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) , Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema takriban wananchi 5,000 wamepatiwa huduma za afya jumuishi kwa watu wa makundi yote hususan Wanawake, Watoto, Vijana na Watu wenye ulemavu kupitia kambi za matibabu za Afya Bora, Maisha Bora chini ya ZMBF.
Mariam Mwinyi amesema hayo alipozindua Kampeni ya "We
Are Equal" (yaani kwa Kiswahili Tupo Sawa) inayoratibiwa na Taasisi ya Maendeleo
ya Wake wa Marais wa Afrika (OAFLAD) na kufunga kambi ya nne ya matibabu ya
"Afya Bora, Maisha Bora" katika Viwanja vya Hospitali ya
Kitogani, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe
28 Februari, 2025.
Aidha , Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania inakuwa nchi ya
22 kuzindua Kampeni hii kati ya nchi 54. Ambayo ndio nchi ya mwisho kuzindua
katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa kampeni hii.
Halikadhalika, Mariam Mwinyi amesema Kambi ya Matibabu
inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya
Zanzibar Maisha Bora Foundation katika kuunga mkono juhudi za Kampeni ya
#WeAreEqual kwa kutoa huduma jumuishi katika kuimarisha ustawi wa jamii kufikia
wananchi 21,000 hadi sasa.
Mariam Mwinyi ametoa wito kwa wananchi wote kupaza sauti
dhidi ya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia na changamoto zote zinazo
kwamisha maendeleo ya Wanawake na Wasichana.
Naye, Mke wa Rais wa Kenya Mama Rachel amempongeza Mama
Mariam Mwinyi kwa kuzindua Kampeni hii kwa ustawi wa maendeleo ya Wazanzibari
na Afrika kwa ujumla.
Vilevile, Mke wa Rais
wa Burundi Mama Angeline Ndayishimiye
amefurahia kujumuika na Mama Mariam Mwinyi katika uzinduzi wa Kampeni hii na
kusisitiza kuwa sisi sote wana Afrika mashariki ni wamoja.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi zisizo za Serikali, wadau wa maendeleo wameshiriki uzinduzi huu pia Mwakilishi wa Mke wa Rais wa Angola na Nigeria pamoja na Katibu Mtendaji wa OAFLAD , Dk. Nardos Berhanu.
0 Maoni