WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 08, 2025 ni mgeni
rasmi katika maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Anwani za Makazi inayofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC), Jijini Dodoma.
Utekelezaji wa oparesheni ya mfumo wa anwani za makazi
nchini umewezesha ukusanyaji wa taarifa milioni 12.3 za anwani za makazi ambazo
zimehifadhiwa katika mfumo wa kidijitali unaojulikana kwa jina la National
Physical Addressing (NaPA).
Mfumo wa anwani za makazi ni daftari la kidijitali la wakazi
na makazi kwa ajili ya ambalo linawezesha kuharakisha na kurahisisha
upatikanaji wa huduma za kijamii na kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama,
kuchochea ukuaji wa uchumi, kuwezesha biashara mtandao na kufanyika kwa ufanisi
pamoja na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na majanga.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “tambua na tumia anwani za makazi kurahisisha utoaji na upokeaji wa huduma”.
0 Maoni