Serikali imekanusha madai ya uwepo wa uhaba wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV) na kuwatoa hofu watumiaji wa dawa hizo kwa kusema kwamba dawa za ARV zipo za kutosha nchini.
Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Afya, imesema kwamba
taarifa hizo za upotoshaji zimeleta hofu miongoni mwa wananchi na kusababisha
baadhi ya wagonjwa kuomba dawa za muda mrefu ili waweke akiba.
"Kitendo cha wagonjwa kutaka kupewa dawa za muda mrefu ili waweke akiba, si sahihi na kinaweza kuathiri utunzaji na matumizi sahihi ya dawa," imesema taarifa hiyo iliyotolewa na Roida Andusamile Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya.
Kuibuka kwa madai ya uhaba wa ARV, kunafuatia uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha shughuli za Shirika la Marekani la USAID pamoja na ufadhili wa dawa hizo kwa mataifa ya Afrika, na kuzitaka nchi hizo zijitegemee.
0 Maoni