Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepanga kutoa matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo
ya mishipa ya damu kutanuka kwenye miguu kwa jina la kitaalamu ‘Varicose Vein’
katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya kutanuka kwa mishipa hiyo.
Taarifa
iliyotolewa na JKCI imesema kwamba matibabu hayo yatakayotolewa kuanzia tarehe
12 hadi 15 Februari 2025 na yatafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na
wenzao kutoka Hospitali ya Andalusia ya nchini Misri.
JKCI imewaomba
wataalamu wa afya nchini kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa kuwatuma
wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu kutanuka kwenye waje kutibiwa katika
kambi hiyo maalumu na kupatiwa tiba.
Matibabu
yatakayofanyika katika kambi hiyo ni ya upasuaji kwa njia ya kutumia matundu
madogo katika kutibu mishipa ya damu ya vein iliyotanuka kwa kutumia kifaa cha
umeme kijulikanacho kwa jina la laser ablation machine, imeeleza taarifa
hiyo ya JKCI.
0 Maoni