Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mkoani
Geita Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa
nia, dhamira na Upendo wake kwa wakazi wa Bukombe hasa kwa namna ambavyo
amekuwa chachu ya maendeleo kwenye Jimbo la Bukombe.
"Nimshukuru
sana Mhe. Rais kwa mapenzi makubwa na kwa maendeleo makubwa tuliyoyapata, Ninyi
ni mashahidi kwa kazi kubwa nitakazozieleza hazitokani na jambo lolote
isipokuwa yeye mwenyewe kuweka msisitizo kwenye kazi hizi na ndio maana Mkutano
mkuu wa Chama uliamua kwa kauli moja kumteua moja kwa moja kuwa Mgombea kwenye
uchaguzi ujao." Amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko
akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020-2025
kwenye Jimbo la Bukombe Mkoani Geita, leo Februari 08, 2024 mbele ya Mgeni
rasmi Rais mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
0 Maoni