Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima
amekemea vikali ongezeko la wimbi la maudhui yasiyofaa yanayosambazwa mtandaoni
yakionesha baadhi ya mambo yasiyofaa wala kuzingatia weledi.
Dkt.
Gwajima ametolea mfano wa mzalishaji maudhui mmoja ambaye hivi karibuni ameonekana
akisambaza maudhui ya kuuza figo za mtoto, mwingine akionesha maudhui ya
kuandaa vinywaji na vyakula vichafu na kujitapa kuwa anawauzia wananchi wa
Kariakoo na wa maeneo mengine.
Maudhui
mengine yaliyokemewa na Dkt. Gwajima ni ya wale wanaosambaza maudhui ya kufanya
mapenzi hadharani yakiwemo ya jinsia moja, wengine wakisambaza maudhui kuhusu
fursa za kujipatia fedha kwa njia zisizoeleweka.
Waziri
Gwajima amewataka Watengeneza maudhui kuzingatia weledi na miongozo yote na
kama Mtu hana elimu na ufahamu kuhusu kuandaa maudhui ya mtandaoni aache mara
moja kwakuwa ataharibu na atawajibishwa ambapo amewataka wale wote ambao
wamepakia maudhui kinyume na miongozo husika wayafute haraka maudhui hayo
mtandaoni.
0 Maoni