Wachezaji Singida Black Stars ni raia wa Tanzania kwa tajnisi - Uhamiaji

 

Idara ya Uhamiaji imetoa ufafanuzi kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji wa klabu ya Singida Black Stars, Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana), Josephat Arthur Basa (Cote d'voire) na Muhamed Damara Camara wa Guinea.

Taarifa ya idara hiyo imesema kuwa wachezaji hao watatu waliomba uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357, hivyo ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi.



Chapisha Maoni

0 Maoni