Jeshi la Polisi nchini limewakamata askari wawili wa
kikosi cha usalama bararani waliorekodiwa wakichukua rushwa hadharani kutoka wa
madereva wa daladala na kusema kuwa watachukuliwa hatua za kali za kinidhamu za
mashtaka ya kijeshi.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema kwamba
askari hao mmoja mwanaume na mwingine mwanamke tayari wamekamatwa na wapo
mahabusu.
0 Maoni