Mwandishi wa Habari Eugen Peter ambaye leo asubuhi kupitia kurasa za @millardayo alitangazwa kutokujulikana aliko, amepatikana leo mchana akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa MOI, Eugen alifikishwa Hospitali hapo Desemba 31, 2024 akitokea
Hospitali ya Mwananyamala akiwa amepoteza fahamu na akiwa na majeraha mikononi
na kichwani yanayotajwa kuwa yamesababishwa na ajali ya pikipiki ambapo
alilazwa kama mgonjwa asiyejulikana utambulisho wake (unknown patient).
Eugen
ambaye wakati wa kutoweka kwake alikuwa amechukua likizo ya kazi mwishoni mwa
mwezi Desemba, hakwenda nyumbani kwao Arusha kama ilivyotarajiwa wala
hakuonekana nyumbani kwake Ubungo na simu zake hazikuwa zikipatikana ndipo ndugu,
jamaa na marafiki wakishirikiana na Ofisi yake (AyoTV) walipoanza kumtafuta
katika maeneo mbalimbali.
AyoTV
imetoa shukurani kwa wote walioshiriki katika jitihada za kumtafuta na wale
wote waliofanikisha kupatikana kwake ikiwemo Taasisi ya MOI.
0 Maoni