Muonekano wa Mlima Kilimanjaro leo

 

Muonekano wa leo Januari 20, 2025 wa Mlima Kilimanjaro kwa upande wa pili kutokea kijiji cha Kamwanga kilichopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Unapokuwa katika eneo hili maarufu kwa kilimo cha Viazi mviringo utakiona kilele cha Mawenzi chenye urefu wa mita 5149 upande wa kushoto mwa kilele cha Kibo chenye urefu wa mita 5895.

Kwa upande wa Magharibi wa kilele cha Kibo kuna tambarare nzuri ya Shira yenye urefu mita zaidi ya 3900 huku ikiwa na utajiri wa msitu mnene wenye miti aina ya Campher na Podo yenye mchango mkubwa wa kuvuta mvua kwa upande wa Magharibi mwa Mlima Kilimanjaro.

Aidha, kijiji hiki cha Kamwanga ni miongoni mwa maeneo machache mkoani Kilimanjaro ambayo huupa Mlima Kilimanjaro muonekano wa kuvutia huku ukikipamba kilele cha Kibo kwa kuwa katikati ya vilele viwili vya Shira kwa upande wa Magharibi na Mawezi kwa upande wa Mashariki.



Chapisha Maoni

0 Maoni