Moto wanyika waua watu 16 hadi sasa Los Angeles

 

Watu wapatao 16 wamekufa kwa moto wa nyika Los Angeles hadi sasa, ambapo 11 katika eneo la Eaton na watano huko Paisades, huku wengine 13 hawajulikani walipo.

Mji wa Malibu umeathirika kwa moto huo katika eneo la mashariki, Meya wa mji huo amesema na kuongeza kuwa kuibuka kwa upepo kutatatiza jitihada za kuzima moto.

Moto mkubwa wa Palisades, unasambaa mashariki na sasa unatishia makazi ya matajiri ya Brentwood, ambapo mari ya watu kuhama imetolewa.



Chapisha Maoni

0 Maoni