Moto waelekea kuteketeza alama ya Hollywood

 

Moto umetokea katika vilima vya Hollywood na unaelekea kufika kwenye alama maarufu ya Hollywood, wakati ambapo majengo kwenye mji wa Sunset Boulevard wa eneo hilo maarufu kwa filamu na burudani yakiteketea kwa moto. 

Mkuu wa Zimamoto amewaambia waandishi wa habari kuwa moto huo unaongezeka kwa kasi, na hakuna uwezekano wa kuudhibiti.

 Nyumba ya Paris Hilton ni miongoni mwa nyumba za nyota wa hadhi ya juu ambazo zimeungua moto. Watu wanatano wameripotiwa kufa huku wengine zaidi ya 137,000 wamehamishwa makazi kuepuka janga hilo kubwa kuwahi kutokea Los Angeles.

Chapisha Maoni

0 Maoni