Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi
kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Jijini Dodoma kwa
kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuongeza kipato chao.
Mh. Mavunde ametoa ahadi hiyo leo wakati wa Mkutano wa
Kikundi cha Twiga cha wafanyabiashara wadogo wadogo uliofanyika ndani ya Soko
la Sabasaba.
“Tunaishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu yanayoendelea ndani ya
Jiji la Dodoma,” alisema Mh. Mavunde.
“Nipo hapa leo kama Mwanachama mwenzenu wa kikundi cha Twiga
ambacho tulikiasisi pamoja. Nina furaha kubwa kusikia mipango iliyopo ya
kuongeza miradi ya kujiimarisha kiuchumi, nitajitahidi kuendelea kuwashika
mkono ili muweze kusimama kiuchumi.”
Pamoja na mradi wa Shamba la mbogamboga
nililowapatia,nitawaongezea na mradi wa kutoa huduma ya maji safi kwa
wafanyabiashara wa soko la Sabasaba,TV ya inchi 55 kww ajili ya mradi wa
kuonesha mpira na Shilingi Milioni 5 kutunisha mfuko wa Kikundi, alisema
Mavunde.
Akitoa shukrani kwa niaba Mlezi wa Kikundi cha Twiga Mama Anna Nyigana amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwajali na kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara hao wadogo na kuahidi kusimamia ipasavyo miradi hiyo ili iweze kuleta tija ya kiuchumi kwa wanakikundi.




0 Maoni