Mkutano baina ya Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi
Yakubu na Viongozi wa Umoja wa Madereva
nchini humo ambapo viongozi hao wamefika kuangalia fursa za ushirikiano na
wenzao wa Tanzania ikiwa ni pamoja na mafunzo hususan kwa vyombo
mahsusi,upatikanaji wa vipuri vya magari na fursa za ajira kwa wanachama wao.
Kwa upande wake Balozi Yakubu aliwaahidi viongozi wa
Umoja huo ambao unajumuisha madereva wote nchini Comoro kwa visiwa vyote kuwa
watawatafutia Taasisi mahiri za udereva ili washirikiane nazo ikiwemo Taasisi
za Serikali kwa mafunzo wanayohitaji.



0 Maoni