Marekani haitatekeleza ongezeko la kodi kwa Colombia, baada ya taifa hilo kuufyata na kukubali kuwapokea wahamiaji wanaohamishwa kwa nguvu kutoka Marekani.
Rais Donald Trump aliagiza ongezeko la kodi la asilimia 25 kwa bidhaa zote zinazozalishwa Colombia, baada ya Rais wa taifa hilo kuzuia ndege zenye wahamiaji kutua nchi hiyo Jumapili.
Rais wa Colombian Gustavo Petro amesema atakubali kuwapokea
wahamiaji raia wa nchi hiyo wakiwa kwenye ndege za kiraia na bila kuwachukulia
kama wahalifu.
Taarifa ya Ikulu ya Marekani imesema kuwa Colombia imekubali kuwapokea wahamiaji wanaowasili kwa ndege za Marekani, “bila vikwazo wala kuchelewesha.”

0 Maoni