Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Serikali haiko tayari kuona maisha ya Watanzania yanawekwa rehani kwa uzembe wa madereva na wasafarishaji wenye tabia ya kwenda mwendokasi, kujaza abiria kupita kiasi, kunywa pombe wakati wakiendesha vyombo vya moto na tabia nyingine za aina hizo zinazokiuka Sheria za Usalama Barabarani.
“Ole wake atakayebainika kusababisha ajali za kizembe,
Serikali haiko tayari kuona maisha ya Watanzania yanawekwa rehani kwa uzembe wa
watu wachache,” amesisitiza Bashungwa.
Bashungwa ametoa wito kwa wasafiri na wasafirishaji,
kuzingatia na kuheshimu Sheria za Usalama Barabarani, ili kupunguza ajali
zinazoepukika, ambazo mara nyingi zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na hata
kusababisha ulemavu kwa wananchi wenzetu.
“Yapo matukio ya ajali ambayo yanatokana na uzembe wa
madereva ama wamiliki wa magari kutofanyia matengenezo ya mara kwa mara vyombo
hivyo vya usafiri,” ameeleza Bashungwa.
Bashungwa amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua kali
kwa madereva na wasafarishaji wazembe kwani Sheria za kudhibiti uzembe zipo.
Aidha, Bashungwa ametoa tahadhari kwa familia zinazotumia
magari yao binafsi, kuacha utamaduni wa kuchukua mtu yeyote ambaye hana taaluma
ya udereva wala hajapitia mafunzo ya kuendesha magari kwa kukwepa gharama.
0 Maoni