Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi, aliyeripotiwa kupotea
tangu Desemba 11, 2024 imebainika amekufa na mwili wake inasemekana umekutwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Baba mkwe wa Ulomi, Japhet Munisi amenukuliwa akisema alipigiwa simu leo asubuhi na mke wa marehemu, akimjulisha kuwa amepata taarifa kuwa mwili wa mumewe upo hospitali hiyo.
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa akifanya biashara za fedha
za mitandao ya simu maeneo ya Sinza Kijiweni na Mwenge alipotea tangu Tarehe 11
Desemba 2024.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam bado halijatoa taarifa rasmi kuhusiana na kupatikana kwa mwili wa Ulomi.
Awali Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lilisema
Desemba 12, 2024 katika kituo cha Polisi Chang'ombe, Temeke ilipokelewa taarifa
ya kutafutwa na familia yake mtu aitwaye Daisle Simon Ulomi, mfanyabiashara
ambaye hakurudi nyumbani kwake tangu alipoingia kazini kwake Desemba 11, 2024.
0 Maoni