Waziri wa
Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema Serikali inatumia shilingi 400,000 kwa
Mtanzania mwenye maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kila mwaka ikiwa ni sawa
na Shilingi bilioni 750 kwa WAVIU milioni 1.7 waliopo nchini.
Waziri
Jenista amesema hayo leo Desemba Mosi, 2024 kwenye kilele cha maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Duniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa mjini Songea mkoani
Ruvuma, katika viwanja vya Maji Maji huku Makamu wa Rais, Dk Isdory Mpango
akiwa mgeni rasmi.
"Inakadiriwa
kila mwaka kila mtu anayeishi na VVU katika Taifa letu anatumia fedha
zisizopungua Shilingi 400,000 na kama tunavyojua wenye maambukizi ni milioni
1.7 nchini, hivyo tukitumia zaidi ya Shilingi bilioni 750 kila mwaka
kuhakikisha tunafubaza VVU na UKIMWI ndani ya Taifa letu," amesema Waziri
Jenista.
"Gharama
hii ni kubwa, tuna kila sababu kuzuia maambukizi mapya nchini na kuhakikisha
walio katika dawa wanafubaza virusi vya kwa kutoa tiba stahiki na kuhakikisha
WAVIU wote wanaendelea kufubaza VVU na wataendelea kulindwa katika uhai
wao," ameongeza Waziri Jenista.
Aidha,
Waziri Jenista ametoa wito kwa jamii kuepuka tabia ambazo zinatajwa kuwa
viashiria na chanzo cha maambukizi mapya ikiwemo unywaji wa pombe kupindukia,
kuwa na wapenzi wengi pamoja na ngono zembe.
Na. WAF -
Ruvuma

0 Maoni