Tanzania imepiga hatua kubwa matumizi gesi asilia - Dkt. Biteko

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika huduma za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme unaotokana na gesi asilia.

Dkt. Biteko ameyasema hayo katika mahojiano maalum aliyoyafanya hivi karibuni na Shirika la Habari la Utangazaji la Uingereza - BBC, Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Biteko amesema Tanzania inategemea kuunganisha nyumba 1000 na gesi asilia katika mwaka wa fedha 2024/25 na hadi sasa nyumba nyingine 1500 tayari zimeunganishwa na mpango huo.

Ameeleza kuwa kama taifa, Tanzania imepiga hatua kubwa, kwa kuweka uwekezaji mkubwa sana katika uzalishaji vyanzo vingi vya umeme, ambapo kwa sasa inaziada ya umeme wa zaidi ya Megawati 740.

“Kwa kuwa maendeleo yanaendelea kuwa makubwa na ongezeko la mahitaji ya umeme linahitajika, bado tunahitaji kuwa na vyanzo vingi zaidi, ndio maana leo tunajenga miradi ya solar (umeme jua) Kishapu, Rumakali na tujenge miradi mingine ya gesi,” alisema Dk. Biteko.

Chapisha Maoni

0 Maoni