Mamia ya watu wanahofiwa kufa katika kisiwa cha Mayotte
cha Ufaransa kilichopo bahari ya Hindi, baada ya kukumbwa na kimbunga Chido chenye
kasi ya kilomita 225 kwa saa.
Kiongozi wa kisiwa hicho cha Mayotte amesema idadi ya
waliokufa, inaweza kufikia karibu watu elfu moja ama maelfu kadhaa.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa ameanza safari kuelekea
katika kisiwa hicho, akiwa na askari wa zimamoto wapatao 160.
Kisiwa cha Mayotte ni moja ya eneo masikini la Ufaransa,
ambapo wengi wa wakazi wake 300,000 wanaishi kwenye nyumba za mabanda.
Mmoja wa wakazi wa Mayotte, amesema kwamba ameshuhudia
makazi yote ya majirani zake yakitoweka.
0 Maoni