Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, aliyetokea
familia ya hali ya chini akiwa ni mkulima wa karanga, amefariki dunia akiwa na
umri wa miaka 100.
Katika utawala wake wa muhula mmoja akiwa madarakani
alifanikiwa kupatikana kwa amani baina ya Misri na Israel.
Pia alifanikisha kuokoa uchumi uliyokuwa ukiyumba wa
Marekani, pamoja na jaribio hatari la kuwakomboa mateka Wamarekani waliokuwa
wanashikiliwa nchini Irani.
Katiba maisha yake ya baadae alikuwa akijishughulisha
bila ya kuchoka katika masuala ya amani, mazingira na haki za binadamu, jambo
lililomfanya apate tuzo ya Amani ya Nobel 2002.
0 Maoni