Rais Samia atoa msamaha kwa wafungwa 1,548

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza msamaha kwa wafungwa 1,548 ambapo kati yao wafungwa 22 wameachiliwa huru leo Desemba 09, 2024.

Taarifa iliyotolewa leo imesema wafungwa 1,526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

Kupitia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Serikali imesema msamaha huo wa Rais Samia ni sehemu ya kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

“Ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa walioachiliwa huru leo watarejea tena katika Jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.” imesema taarifa hiyo.






Chapisha Maoni

0 Maoni