Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus M. Wambura amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kumhamisha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ramadhani Ng’anzi kutoka kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania kwenda Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Maadili ya Jamii.
Katika mabadiliko hayo mafasi ya (DCP) Ramadhani Ng’anzi
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda
ambaye alikuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
Pia, amemhamisha aliyekuwa Mkuu wa Usalama Barabarani
Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniphace Mbao kutoka Dodoma
kwenda kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es Salaam.
Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Elimu kwa Umma Kikosi cha
Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Michael Deleli
amemhamishia Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Kaimu Mkuu wa Maadhimisho ya
Kitaifa.
Naye Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassoro Sisiwaya
aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, amemhamishia
Mkoa wa Kilimanjaro kwenda kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro.
0 Maoni