Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto
Biteko ameshiriki hafla ya uwekaji Wakfu Jengo la Kanisa la Waadventista wa Sabato
Magomeni inayofanyika leo Desemba 15, 2024 jijini Dar es Salaam.
Dkt. Biteko amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Kanisa hilo limewekwa Wakfu na
Mchungaji Joel Okindo, Msaidizi wa Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki
na Kati (ECD).
0 Maoni