Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ametembelea maabara ya ithibati
ya mazao ya nyuki inayosimamiwa na Taasisi
ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia Kituo chake cha
Utafiti wa Wanyamapori Njiro ambacho kimejikita kwenye utafiti wa nyuki na
mazao yake.
Mhe. Chana
ametoa wito wa kukamilisha maabara hiyo ambayo itaongeza pato la taifa kwa
kupata fedha za kigeni kupitia soko la kimataifa la mazao ya nyuki ikiwemo
asali. Pia uchumi wa mtu moja kwa moja kwa wananchi.
“Serikali ya
Awamu ya sita chini ya uongozi Shupavu wa Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan
inahakikisha wananchi wananufaika na fursa zilizopo kwenye maliasili ikiwemo sekta
ya nyuki,” amesemwa Dkt. Chana.
Mkurugenzi
waK cha Utafiti wa Wanyamapori Njiro Dkt. Wilfred Marealle amesema maabara hiyo
inakamilishwa kupitia Mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya nyuki
(*Beekeeping Value Chain Support Project - BEVAC*) inatarajia kutoa huduma
mwanzo mwa mwaka 2025 na itasaidia kuharakisha biashara ya mazao ya nyuki
katika soko la kimataifa ambapo awali Serikali ilikuwa inatumia gharama kubwa
kupeleka sampuli nje ya nchi kudhibitisha viwango vya ubora.
“Sample
zilikuwa zinachukua muda mrefu kupata majibu na kusababisha kupoteza soko,”
ameeleza Dkt. Marealle.
0 Maoni